Utafiti wa Kiolezo cha Mtazamo wa LGBTQI+ wa Shirika la F&M Global Barometers wa 2024
Tafadhali jaza utafiti huu unaofanywa na shirika la F&M Global Barometers, ili kutusaidia kuelewa jinsi wewe––kama msagaji, shoga, msenge, mbadili jinsia, basha, na/au huntha (LGBTQI+)–– unavyoona haki za binadamu kwa watu wa kundi la LGBTQI+ katika nchi yako.
Kwa utafiti huu, utaombwa ujibu maswali kuhusu hali yako ya usalama, hofu, kukubalika na matukio ya vurugu na ubaguzi kama msagaji, shoga, msenge, mbadili jinsia, mbasha na/au huntha katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Majibu yako hayatakutambulisha kabisa na yatatumika kwa madhumuni ya utafiti pekee. Hakuna taarifa zinazokutambulisha zitakazoshirikiwa hadharani. Utafiti huu umekaguliwa na kuidhinishwa na Bodi ya Ukaguzi wa Kitaasisi (IRB) ya Chuo cha Franklin & Marshall. Maswali kuhusiana na haki zako kama mshiriki katika utafiti huu pia yanaweza kutumwa kwa Mwenyekiti wa sasa wa IRB kupitia irb@fandm.edu.
Tafadhali tuma maswali au wasiwasi kwa Dkt. Susan Dicklitch-Nelson, Mtafiti Mkuu wa Shirika la F&M Global Barometers, kupitia gbgr@fandm.edu. Kwa maelezo zaidi kuhusu shirika la F&M Global Barometers, tafadhali tembelea www.fandmglobalbarometers.org, na ili uone matokeo kutoka kwa utafiti uliopita uliofanywa mwaka wa 2022, tafadhali tembelea www.lgbtqiperceptionindex.org
Utafiti huu unapaswa kuchukua dakika 2 hadi 5 kuukamilisha.